Tuesday, May 14, 2013

Wanaume halisi ndani ya halisi records wakiwa wanatengeneza nyimbo ya fitina ambayo kwasasa inasumbua sana katika baadhi ya vituo vya redio bongo


Friday, November 16, 2012

VIDEO MPYA YA LWP FT JUMA NATURE

LWP wameachia video ya ngoma yao mpya inayoitwa TATIZO FOLENI waliyomshirikisha Juma Nature. Ni ngoma kali sana. Akiongea na mtandao huu, mmoja wa member,Slotter alisema wao ni mashujaa wa kuachia "ngoma za karne" akiwa na maana kuwa ngoma zao huwa ni bora na zina ujumbe halisi kabisa.

Alizidi kupasha kuwa, ngoma zao kama MKE WA MTU SUMU bado zinaleta maana hadi leo huku akiuhusisha wimbo wao huo na tukio la hivi karibuni lililotokea huko Temeke ambapo watu wawili walinasana walipokuwa wanafanya mapenzi.


Friday, October 12, 2012

NGOMA MPYA YA NATURE NA BABY MADAHA - NARUDI KIJIJINI IMEKAMILIKA

 

Video ya ngoma mpya ya Juma Nature na Baby Madaha inayoitwa NARUDI KIJIJINI imekamilika na imeachiwa hewani sambamba na nyimbo baada ya kukamilika chini ya utayarishwaji wa Mike Tee (Mnyalu) chini ya lebo ya ShowBiz Defined. Ni video kali sana. check mwenyewe utakubali...

Tuesday, October 2, 2012

JUMA NATURE KUACHIA NGOMA NA BABY MADAHA

Juma Nature, Baby Madaha, Mike Tee katika mchakato wa kutayarisha video mpya ya Kibra na Baby Madaha
Imekuwa safari ndefu katika muziki wa Hip Hop kwa Juma Nature kama kiongozi wa kundi mahiri la Hip Hop, Wanaume Halisi. Akiwa na zaidi ya miaka 10 kwenye 'gemu', Juma Nature aka Kibra ni kama veteran katika gemu lakini bado ana 'njaa' ya muziki kama mwanamuziki anayechipukia.

Kwa muda mrefu Wanaume Halisi wamekuwa kimya na hii inatokana na sababu kwamba wamekuwa wakitayarisha nyimbo kwa ajili ya ujio mpya. Na kwa kuthibitisha kwamba huu ni ujio mpya, walimsaini Baby Madaha kama member mpya wa kundi lao na wamefanya ngoma moja matata ambayo itaachiwa  hewani pindi video yake, ambayo inatengenezwa na Mike Tee, itakapokuwa tayari.

Monday, September 24, 2012

UJIO MPYA WA KIUTU UZIMA


Katika hali ya kawaida, Wanaume Halisi ni mojawapo ya makundi tata sana katika ukanda wa muziki wa kizazi kipya. Hii inadhihirishwa na ukweli kwamba kiongozi mkuu wa kundi hilo Juma Nature ni nyota pekee isiyofifia katika sura nzima ya muziki Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

Akiongea nyumbani kwake, Juma Nature alikuwa na haya ya kusema "Mimi sina mengi ila kaeni chonjo kwa ujio wa kiutu uzima"

kwa habari zaidi endelea kutembelea hapa.