![]() |
Juma Nature, Baby Madaha, Mike Tee katika mchakato wa kutayarisha video mpya ya Kibra na Baby Madaha |
Kwa muda mrefu Wanaume Halisi wamekuwa kimya na hii inatokana na sababu kwamba wamekuwa wakitayarisha nyimbo kwa ajili ya ujio mpya. Na kwa kuthibitisha kwamba huu ni ujio mpya, walimsaini Baby Madaha kama member mpya wa kundi lao na wamefanya ngoma moja matata ambayo itaachiwa hewani pindi video yake, ambayo inatengenezwa na Mike Tee, itakapokuwa tayari.
Akiongelea hiyo ngoma Juma Nature alikuwa na haya ya kusema "Watu wengine wanatoka kijijini na kuja mjini wakijua kwamba itakuwa fresh, ila wakishafika mjini mambo yanakuwa ndivyo sivyo, that's why ukaona tumefanya ngoma kama hii. Hii ngoma inamuonyesha mtu aliyetoka kijijini ambako alikuwa fresh tu na mali za kutosha ila akashawishika kuja mjini ambako mchezo ukawa mgumu kwake mwishowe akaharibu, kumbe town kuwa watu wake , wenye mji wao. Baadaye akagundua kumbe Bongo huku cheche, hakumfai, akaamua kurudi zake kijijini alipokuzoea."
![]() |
hii ni katika harakati za utayarishwaji wa video mpaya ya Juma Nature na Baby Madaha |
Katika kutia vionjo ujio wao mpya, Wanaume Halisi walimsaini Baby Madaha ambaye ni zao la shoo maarufu ya Bongo Star Search. Anajulikana zaidi kwa ngoma kali kama Amore na Desperado ambazo zote zimefanikiwa kumuweka juu katika tasnia ya muziki wa Bongo, lakini zaidi anajulikana kwa vituko vyake vya hapa na pale ambavyo vinafanya jina lake kuwa habari ya mujini.
![]() |
Baby Madaha katika pozi |
Kaa tayari kwa ujio mpya, Kaa tayari kwa ngoma mpya ya Juma Nature na Baby Madaha.
No comments:
Post a Comment